• UK
  • 08:17 25 Novemba 2009
  • |    
  • 11:17 25 Novemba 2009

Viza za Uingereza

Sehemu ya viza inahusika na utoaji wa viza, na huwapatia huduma ya viza Watanzania pamoja na watu wengine wanaotaka kwenda Uingereza kwa ajili ya biashara, masomo ama kutalii.

Taarifa muhimu kuhusu viza

Maombi na nyaraka husika za viza hupelekwa Ubalozi wa Uingereza Nairobi kwa tathmini, na kisha viza zitatolewa kwa waombaji waliofanikiwa. Aidha, waombaji wa viza bado wataendelea kushughulikiwa hapa Dar es Salaam. Soma taarifa kamili.

Muda wa kupiga simu za viza

Sehemu ya viza inapokea simu za maulizo kuanzia saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana kwa siku za Jumatatu hadi Alhamis na saa 4:00 hadi saa 5:00 asubuhi kwa siku za Ijumaa. Maulizo ya jumla kuhusu jinsi ya kutuma maombi ya viza yanaweza kupatikana katika tovuti hii. Unaweza pia kutuma ujumbe wa barua pepe moja kwa moja katika Sehemu ya Viza kwa maulizo, na utajibiwa katika siku ya kazi inayofuata. Na kama utakuwa umeshindwa kupata taarifa unayotafuta katika mtandao, tafadhali jaribu kupiga simu kwa kuzingatia muda wa simu uliotajwa.

Vielelezo vinavyohusika na maombi ya viza

Hatutapokea vielelezo vyovyote vile kabla ya mwombaji kutuma maombi yake ya viza. Vielelezo vyote vinatakiwa kuletwa wakati muombaji atakapokuja ubalozini kufuatilia maombi yake ya viza. Mdhamini anatakiwa kutuma vielelezo husika kwa mtu anayemdhamini, ili muombaji mwenyewe ndiyo avilete ubalozini, sambamba na maombi yake.

Hakikisha kuwa unatuletea vivuli tu vya vielelezo halisi ambavyo ungependa kubaki navyo (kwa matumizi yako ya baadaye) - hii ikiwa ni pamoja na pasipoti yako. Ubalozi wa Uingereza utabakia na nakala zote halisi ambazo utakuwa umezileta kimakosa bila kuzitolea kivuli. Aidha, si jukumu letu kukutolea nakala za vivuli kwa ajili ya vielelezo vyako.

Huhitaji kupanga foleni!

Tuma maombi yako ya viza kwa njia ya mtandao, na kimsingi inamaanisha kwamba huitaji kupanga foleni nje ya Ubalozi. Tembelea tovuti hii www.visa4uk.fco.gov.uk na kisha ukamilishe maombi yako ya viza kwa njia hiyo ya mtandao. Hata hivyo bado utahitajika kuja ubalozini kukamilisha maombi yako ya viza - ambapo utapewa miadi kuja ubalozini. Aidha, haitawezekana kuja ubalozini kwa siku za Ijumaa kama haujapangiwa kuja.

Endapo maombi pamoja na vielelezo vya muombaji vitakuwa sahihi, maombi yatafanikishwa katika muda mfupi zaidi. Daima tuma maombi yako ya viza angalau wiki sita kabla ya siku yako ya safari.




Kurudi juu